Huawei yazindua Huawei Nova 7 pro 5G, Nova SE na Nova 7 5G
Hivi juzi kampuni ya kutengeneza simu ya Huawei kutokea nchini China, wamezindua simu tatu Huawei Nova 7 Pro 5G, Huawei Nova SE, na Huawei Nova 7 5G. Kati ya simu zote hizo tatu, Nova SE ndiyo ambayo inasemekana kuwa na gharama yenye unafuu kidogo ukilinganisha na hizo nyingine, lakini hizo mbili ambazo ni Pro, ndio ambazo zinasemekana kuwa na ubora zaidi.
Simu zote hizo tatu, zinakuja na camera nne upande wa nyuma wa simu, na camera moja upande wa mbele, isipokuwa kwa Huawei Nova 7 5G Pro ambayo yenyewe inakuja na camera mbili (double camera) kwa upande wa mbele.
Huawei NOVA 7 5G PRO
Simu hii itakuwa inauzwa kwa gharama ya $520 yenye 8GB RAM na 128 ROM (Internal Memory) na $570 kwa yenye 8GB RAM na 256 ROM.
Simu hii itakuja na muonekano wa rangi tatu, rangi ya purple (zambarau), silver, nyeusi na nyekudu. Ukitaka kufahamu zaidi juu ya simu hii pamoja na specification zake angalia hapa
Huawei NOVA SE
Simu hii itakuwa inauzwa kwa gharama ya $420 ikiwa ina 8GB RAM na 128 GB ROM. Camera ya mbele ya simu hii inakuja na 16 mega pixels, na uwezo wake wa battery ni 4000 MAh, pia inakuja na rangi mbalimbali; specification za simu hii unaweza kuzipata hapa
Huawei NOVA 7 5G
Simu hii inakuja na rangi tano, kijani, blue, nyeusi, silver na nyekundu. Itakuwa inauzwa $450 kwa yenye 8GB na 128 GB RAM na kubwa yake itauzwa $480 kwa yenye 8GB RAM na 256 ROM. Specification zaidi za simu hiyo unaweza kuzisoma hapa
No comments