Header Ads

Breaking News

Jinsi ya kudownload video za Tik Tok bila kuwa na watermark wala username

Mtandao wa TikTok ulikuwepo tangu muda mrefu kwenye PlayStore na Appstore, lakini hivi karibuni umeonekana kupata umaarufu mkubwa zaidi baada ya janga hili la corona na hivyo watu wengi wamekuwa wakijifungia ndani ili kuepuka mikusanyiko, na hivyo wengi wao huwa hawana mambo mengi ya kufanya. Kwa kutumia mtandao huo, wengi hutumia kama sehemu ya kujiliwaza, wakiangalia video za watu wengine, wachekeshaji, wasanii, na mara nyingine hata wao wenyewe wamekuwa wakitumia mtandao huo kwa ajili ya kujirekodi na kuweka video zao katika mtandao huo. 

Licha ya kuwa video za TikTok zinaweza kupakuliwa, watu wengi wamekuwa hawazipendi kutokana na video hizo kuonyesha logo ya mtandao huo, pamoja na username ya aliyerekodi video hiyo, jambo ambalo sio watu wengi wametokewa kuvutiwa nalo, kwasababu kuna baadhi ya watu huwa wanapenda usiri (privacy) katika maisha yao. 

Leo tutaangalia ni kwa namna gani tunaweza kupakua video hizo bila kuwa na logo hiyo ya TikTok pamoja na username ya aliyerekodi video hiyo. Unaweza kuangalia video hiyo, hapa chini 

Na hivyo ndivyo ambavyo unaweza kupakua video hizo bila kuwa na logo ya TikTok wala username. Unaweza kuipata application hiyo katika PlayStore na application hiyo ni free

LINK MAALUM
Price: FREE

No comments