Header Ads

Breaking News

Unayopaswa kufahamu kuhusu iPhone 12 Tetesi, Uwezo, Bei na Design

Watu wengi duniani kote ambao ni wapenzi wa bidhaa za kampuni ya Apple, kwasasa wamekuwa wakisubiri kwa hamu ujio wa toleo jipya la iphone 12 ambayo simu hiyo ilibidi iingie sokoni mnamo mwezi wa tatu lakini kutokana na janga linaloendelea la corona, ilibidi uzinduzi huo uhairishwe kutokana na sababu mbalimbali za kibiashara hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu. 

Kama tetesi zitakuwa ni za ukweli, tutegee kuiona iPhone 12 ikija na matoleo manne tofauti yatakayokuwa yanatofautiana kibei lakini pia hata katika uwezo wa kiutendaji.  iPhone 12 Max na iPhone 12 Pro zote zinatarajiwa kuja na kioo chenye inch 6.1 huku iPhone 12 Pro Max inatarajiwa kuja na kioo kikubwa zaidi chenye inch 6.7. Lakini iPhone 12 yenyewe ambayo ndiyo inatarajiwa kupata umaarufu mkubwa zaidi, inatarajiwa kuja na kioo chenye inch 5.4.




Simu hiyo (iPhone 12) inatarajiwa kuuzwa $649 bei ambayo wengi wamesema kuwa itakuwa na unafuu ukilinganisha na ubora wake. Simu hiyo inatarajiwa kuja na chip mpya kabisa kwa ajili ya operation ambayo ni A14 Bionic Chipset na itakuwa na internet speed ya 5G. 

Lakini nini cha tofauti ambacho wapenzi wengi wa bidhaa hizo wakisubirie ambacho pia kitaleta utofauti na kuonesha ubora wake kupitia simu hiyo? Moja kati ya wachambuzi wa wa maswala ya kiteknolojia ametengeneza video ili kuonesha angalau watu wapate taswira ya muonekano na nini wakitegemee kutoka kwenye simu hiyo:
iPhone 12 inatarajiwa kuja na muonekano wa tofauti ukilinganisha na iPhone 11, na nyuma itakuwa na camera mbili (dual camera) na speed ya 5G kwa ajili ya mtandao. Pia simu hiyo inatarajiwa kuja na display nzuri ya AMOLED kama ilivyo kwenye simu nyingi za Samsung.
Lakini kuna mengi ya kuvutiwa nayo kutoka kwenye simu hii. Licha ya kuwa na kioo kidogo ukilinganisha na simu nyingine, upya wa design yake ya sasa ni mzuri unaotaka kufanana na ule wa iPhone SE au iPhone 5S ambao unamfanya mtumiaji kuvutiwa nao lakini pia unafanya simu iwe ya kustarehesha.
Huku wapinzani wa simu hiyo ikiwemo kampuni ya Google ambayo nayo inatarajia kuzindua Google Pixel 5 kipindi hichohicho na kwa bei hiyohiyo, Apple inasemekana kwamba ndiyo ambayo italiteka soko huku wengine wakiwa na mawazo tofauti kwani watumiaji wa Android ni wengi kuliko wanaotumia iPhone. Nini maoni yako, tuandikie hapo chini.

No comments