Header Ads

Breaking News

Samsung yaonya kuwa huenda mauzo yao ya simu na Tv yakaporomoka kwa kiasi kikubwa

Kampuni ya Samsung imesema kwamba biashara yake ya memory card au memory chip kama wengine wamavyopenda kuziita itapata faida kubwa katika kipindi kwasababu watu wengi wanafanya kazi zao nyumbani, lakini biashara zao na bidhaa wanazozitegemea kwa ukubwa sana kama vile simu pamoja na Tv huenda zikafanya vibaya sokoni, ikiwa na maana kwamba huenda zisilete faida katika mwaka huu

Samsung walizindua simu zao mbili mpya hivi karibuni Samsung S20 pamoja na Samsung Z Flip, hata hivyo bado hazikuweza kuongeza mauzo katika kampuni hiyo kwasababu ya ugonjwa wa corona ambao umeonekana kutikisa uchumi wa dunia nzima. 
Kampuni hiyo ambayo pia inafanya biashara ya kuuza memory chip, imesema kwamba hivi karibuni biashara hiyo imeonekana kufanya vizuri sana sokoni kwani server nyingi pamoja na computer zinahitaji storage ya kutosha hususani kipindi hiki ambacho watu wengi wanafanya kazi nyumbani kuepuka ugonjwa huo ambao umeshaua watu wengi duniani mpaka hivi sasa. 

Aidha kampuni hiyo imesema kwamba bidhaa kama vile simu janja (smartphone) pamoja na smart TV zake huenda zikapitia kipindi kibaya sana cha mauzo kwani maduka pamoja na biashara nyingi sana zimetokea kufungwa katika kipindi cha janga hili la corona na hivyo kupunguza mauzo ya bidhaa hizo, huku pia uwekezaji wa network ya 5G ambayo inaendelea kufungwa katika nchi ya korea na pande nyingine za dunia, umepungua.
Licha ya hali hiyo kuwepo, kampuni hiyo imesema kwamba itatengeneza namna ya kuwafanya wateja wake wafanye manunuzi katika mtandao (online) kwani wengi wanashindwa kutoka kwenda kwenye stores kwa ajili ya kununua bidhaa hizo kutokana na hali iliyopo. Aidha, Samsung wamesema pia watajaribu kuongeza bidhaa mpya nyingi ili kuwafanya wateja wavutiwe zaidi ili kuongeza mauzo. 
Virus hiyo mpya aitwae corona, anayesababisha ugonjwa unaoitwa COVID-19 aligundulika mwaka jana mwezi Desemba katika mji wa Wuhan ulioko nchini China, na tangu hapo ameleta madhara duniani kote, kwani mpaka sasa zaidi ya watu milioni tatu wameshaathirika na ugonjwa huo na zaidi ya watu laki 5 wakeshafariki hadi sasa, huku madhara mengine yakiwa miji kufungwa, ibada kutofanyika, shule kufungwa, biashara kusimama pamoja na kuporomoka kwa uchumi.

No comments