Unayopaswa kufahamu kuhusiana na ubora wa iPhone SE (2020)
Wengi watakuwa wanafahamu kuwa hivi karibuni kampuni ya kutengeneza simu maarufu kama Apple, ilizindua simu mpya inayofahamika kama iPhone SE (2020). Labda nikurudishe nyuma kidogo, iPhone SE ilitoka kwa mara ya kwanza mwaka 2016, ikiwa ni mwendelezo wa kizazi cha iPhone 5, 6s na 7. iPhone SE ilikuwa ni ya aina yake na kitu ambacho watu wengi walifanya waipende zaidi ni kwasababu ilikuwa na specification kama za iPhone 6s huku ikiwa na umbo kama la iPhone 5 au 5s.
Na miaka minne sasa imepita na Apple wameamua kutoa mwendelezo wa iPhone SE kwa kutoa iPhone SE (2020) ambayo pia inafahamika kwa jina la iPhone SE 2. Simu hii inakuja na umbo kama la iPhone 8 ikiwa na maana kwamba kioo cha simu hii kitakuwa na inchi 4.7 pamoja na home button, lakini haitakuwa na Face ID kama ilivyo iPhone X na iPhone 11.
Apple waliamua kutengeneza simu hii kwani wateja wengi ambao walikuwa wanatumia iPhone 6 pamoja na 6 plus, walishindwa kununua simu mpya kwa kuwa gharama zilikuwa kubwa. Na kama pia unafahamu ni kwamba Apple baada ya kutambulisha software update yao iOS 13 simu za zamani nikiwa na maana ya iPhone 5,5c,5s,6 na 6 plus hazikuwekewa uwezo wa kudownload software hiyo mpya.
Kupitia iPhone SE sasa wateja wanaomiliki simu za zamani kama hizo ambazo nimekwisha taja, Apple wanatarajia wateja hao kununua simu hizo mpya kwa wingi kwani gharama zake ni nafuu sana na mteja atapata mambo yote mapya. Hizi hapa ni specification za simu hiyo unaweza kuziangalia hapa
Lakini pia hapa chini nimeweza kukuwekea video, kama wewe unahitaji kununua simu hiyo, basi unaweza kujionea ubora na uimara wa simu hiyo kwa vitendo ili uwe umejiridhisha na bidhaa ambayo unahitaji au unatarajia kununua. Apple wanaiuza simu hiyo kwa kiasi cha $399 na hivi karibuni simu hizo zitaanza kuingia nchini Tanzania, zikiwa tayari kwa ajili ya mauzo.
Unaweza kutuandikia maoni yako kuhusu simu hiyo katika comments section hapo chini:
No comments