Header Ads

Breaking News

Roboti anaesaidia kupambana na Corona huko Marekani

Ni ukweli usiopingika ya kwamba kwa sasa dunia nzima inapambana na janga la corona, ambalo mpaka sasa limeshaathiri watu wengi sana, takwimu zinaeleza kuwa kumekuwa na visa zaidi ya milioni mbili hadi sasa na vifo zaidi ya laki 2 duniani kote.

Huko nchini Marekani, idadi ya madaktari, manesi na wasaidizi wengine takribani 5,400 ambao walikuwa wanasaidia wagonjwa kupambana na COVID-19 (coronavirus), habari mbaya ni kwamba ugonjwa huo umetokea kuwaathiri hata wao wenyewe na mamia ya maprofesa wameshafariki hadi sasa kutokana na ugonjwa huo. Ni ukweli usiopingika ya kwamba kupambana na virus ambae anaweza akaishi kwa muda mrefu kama corona, anayeweza kuambukizwa kwa njia ya hewa na matone ya majimaji kutoka kwa mgonjwa ni jambo gumu sana na linahatarisha maisha.

Kupitia hilo, baadhi ya hospitali huko Boston, kupitia maombi waliyoyapata kutoka kwa baadhi ya madaktari, wametengeneza mbwa wa kiroboti anayejulikana kama Spot.

Taasisi ya Boston Dynamics ambao ndio watengenezaji wa maroboti hao walisema "Kuanzia mwezi Machi, tulianza kupokea maombi kutoka katika baadhi ya hospitali ambazo zilitusihi kama maroboti tunaowatengeneza wanaweza kufanya jambo lolote kusaidia katika kipindi hiki kigumu ili kuepuka wauguzi kuendelea kukumbwa na janga hili la corona.

 Kiujumla, taratibu ni kwamba watu wote ambao wanasemekana kuwa na maambukizi ya corona wanatakiwa wakae nje, takribani mita 5 ili wapimwe joto la miili yao. Zoezi hilo huwa linahusisha madaktari watano katika kila shift ambao wote wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya corona. Kupitia roboti huyo Spot, sasa madaktari hawatahitaji tena kukutana na mgonjwa ana kwa ana kwa ajili ya kutambua hali yake ya kiafya na namna wanavyoweza kumsaidia. 

Jambo hilo limeweza kupunguza sana hatari ya wauguzi kupata ugonjwa huo, japokuwa mbwa hao bado wapo wachache, na hivyo inaonekana uhitaji wao ni wa hali ya juu, kwani wangeongezwa idadi, zoezi hilo la kupima wagonjwa lingeweza kuwa rahisi zaidi. Mbwa huyo wa kiroboti amewekewa iPad katika eneo la uso wake, pamoja na redio katika eneo lake la nyuma na hivyo madaktari wanaweza kufanya video conferencing akiwa na mgonjwa na kumwelekeza anachotakiwa kufanya. 

Taasisi hiyo ya Boston Dynamics, imesema kwamba inatarajia kumwongezea uwezo roboti huyo kwa kutumia teknolojia ya UV-C Light, ili kwamba awe anaweza kuua baadhi ya chembechembe za vijidudu wengine (virus) na kufanya usafi kwa kutumia Sanitizer katika maeneo ya hospitali. 

No comments