WhatsApp imewaonya watuamiaji wake kuhusu wizi wa taarifa unaoendelea mtandaoni
Mtandao wa WhatsApp umetoa taarifa kwa watumiaji wake kuhusu aina mpya ya wizi unaoendelea mtandaoni, unaofanywa na watu wanaodai kuwa ni team ya kiufundi (technical team) kutoka katika mtandao huo, na kuanza kutuma messages kwa watumiaji wa mtandao huo wakihitaji nambari ya ukaguzi (verification code) kutoka kwa mtumiaji. Account hiyo inayotumiwa na watu hao kufanya hivyo imewekewa picha ya logo ya mtandao wa WhatsApp ili mtumiaji anapoamua kutoa namba hizo awe anadhani ujumbe huo aliotumiwa ni kutoka kwa mtandao huo, lakini WhatsApp hapo jana walitoa taarifa kuwa WhatsApp huwa haitumii mtandao huo kwa ajili ya kuwasiliana na watumiaji wake, bali kama kuna jambo lolote, mtandao huo huwa unatumia mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook pamoja na Twitter kutoa taarifa ama kutumia tovuti yao.
Kutokea Twitter, account ya WhatsApp ambayo huwa inatumiwa na mtandao huo kwa ajili ya kuwapa taarifa watumiaji wake juu ya features mpya mbalimbali zilizoongezeka kwenye mtandao huo ijulikanayo kama "WABetaInfo", account hiyo iliweza kushare ujumbe kutoka kwa moja ya watu (Dario Navarro) waliotumiwa message hiyo na wezi hao wa taarifa. Wezi hao hutumia lugha ya kihispania ili kumuomba mtumiaji aweze kuwapa verification code za kwenye account yake ambazo mara zote huwa ni tarakimu sita na hutumwa kwa njia ya message.
This is #FAKE. WhatsApp doesn't message you on WhatsApp, and if they do (for global announcements, but it's soooo rare), a green verified indicator is visible.WhatsApp never asks your data or verification codes.@WhatsApp should ban this account. 😅 https://t.co/nnOehPL8Ca
— WABetaInfo (@WABetaInfo) May 27, 2020
Wengi wanaweza wasifahamu kwanini wezi hao huomba code hizo na wengine wanaweza kudhani kuwa huenda hazina maana yoyote lakini kulingana na mtandao wa WhatsApp, code hizo ndizo hutumika kwa ajili ya kutengeneza account ya mtumiaji mpya, lakini pia hutumika kulinda account ya mtumiaji ili isiweze kuwa hacked.
Aidha mtandao huo umesema kuwa kwa kuwa wezi hao hutumia picha au logo ya mtandao huo, watumiaji wengi ambao hawawezi kutofautisha wanaweza ingia kwenye mtego huo. WhatsApp imewaomba watumiaji wake, kutotoa taarifa zozote zinazohusiana na account zao ikiwa ni pamoja na code hizo. Lakini imeongeza kuwa kama kuna mtumiaji ambae tayari ameshaathirika na tukio hilo, anaweza kurudisha account yake kwa kuomba tena verification code kutoka WhatsApp na wanaweza kumtumia code nyingine mpya.
Hii si mara ya kwanza tukio kama hilo limeweza kujitokeza, na hivyo taarifa hizi zinaweza zisiwe mpya sana maskioni mwa watu, lakini watu wengi wanazidi kuibiwa taarifa zao za muhimu pamoja na account zao. Aina hii ya wizi iliweza kugundulika tangu mwaka 2018 huko nchini Uingereza.
No comments