Header Ads

Breaking News

Jiandae na ujio wa Infinix NOTE 7 hapa Tanzania

Kampuni ya Infinix Mobility, iko mbioni kuleta simu yenye hadhi ya juu Infinix Note 7, na kupewa jina la BIG MAKINI kutokana na kioo chake kuwa na size kubwa 6.95 inch na uwezo wa camera  48MP na processor ya G70 kutoka Mediatek
Processor ya G70 ina uwezo mkubwa wenye kuwezesha matumizi mbalimbali kwa wakati mmoja bila kuchoka, NOTE 7 inatumia OS mpya kutoka Google, Android 10. Simu hii haitazinduliwa rasmi kama utaratibu wao ulivyozoeleka bali kupitia mitandao yao ya kijamii @infinixmobiletz wameeleza sifa na umaradufu wa simu hii. Yawezekana kuwa ndio simu bora zaidi ya Infinix kutoka mwaka huu.
Vilevile tunawashukuru watanzania kwa kuipokea vyema Infinix Note 7 Lite, iliyoingia sokoni katika mwezi huu wa April. Infinix note 7 ni simu inayoweza kumsaidia mfanyakazi katika shughuli zake za kila siku kwani inaweza kutunza kumbukumbu kwa 64 GB ROM ya 4 GB RAM, pia kuna sifa nyingine kama Document Scanning, hivyo huitaji kupakua app ya ziada. Tumeunganisha teknolojia ya kisasa zaidi. Pamoja na sifa zote hizi tumeweka bei ya kawaida kwa mtanzania mwenye kipato cha kati." Aisha Karupa Afisa Mahusiano 

Tunawakaribisha wateja wetu kununua Infinix Note 7 Lite, sasa zipo madukani, na kwa kila mteja atakayenunua  atapata zawadi mbalimbali kutoka Infinix ikiwemo magic cup, notebooks, speaker, vilevile unaweza kujishindia simu nyingine, ila hii itakuwa kwa wale watakaonunua Note 7 kipindi itakapoingia sokoni mwezi ujao

No comments