Google kuja na Subscription plan kwa watumiaji wa Android TV Playstore
Mwaka jana kwenye mkutano wa kuangalia namna gani wanaweza kuboresha mfumo wa Playstore kwenye Smart TV's, kampuni ya Google iligusia pia suala la kuwepo na "Subscription" katika soko hilo la kupakua apps mbalimbali. Tangu kutokea hapo, tumeona maboresho mbalimbali ambayo Google wameendelea kuyafanya, ikiwemo kubadilisha taswira nzima kabisa ya soko hilo la Playstore na kufanya kuwa na muonekano mwingine wa kisasa zaidi. Lakini hivi karibuni kampuni hiyo imesema watu watarajie feature hiyo kuwepo kwani ipo kwenye majaribio hivi sasa na itaweza kuanza kutumika hivi karibuni.
Kupitia sehemu hiyo mpya ya kuchangia (subscription), sehemu hiyo inakuja na option mbili wakati mtumiaji anataka kupakua application kutoka Playstore kwa kutumia TV yake. Option hizo nazo ni "Free Trial & Install" au "Subscribe & Install. Kupitia "Free Trial & Install" mtumiaji ataweza kutumia app husika kwa muda wa kipindi kifupi akiangalia ubora wake na jinsi inavyofanya kazi, kama atapendezwa nayo basi ataweza kuinstall kwenye TV yake baada ya muda huo wa majaribisho kuisha. Kupitia "Subscribe & Install" mtumiaji ataweza kununua app moja kwa moja bila kupata muda wa majaribisho.
Mpaka kufikia sasa, bado hakuna application zinazotumia malipo kwenye simu ambazo zimeanza kutumika kwenye TV, lakini wawakilishi kutoka Google wanasema kuwa feature hiyo ni mpya na hivyo bado haijaanza kuwa rasmi na hivyo watu wategemee kuiona hivi karibuni. Kwa bahati mbaya kampuni hiyo haikuweza kuweka wazi ni application gani ambazo zinafanyiwa majaribio hayo ya malipo kwa sasa, lakini ni jambo la muda tu mpaka hapo itakapokuwa wazi.
Mmoja ya wawakilishi alisema kuwa
"Sikuzote tumekuwa tukifanya kazi kwa kuboresha huduma zetu ili kumpa mteja urahisi wa kufanya mambo yake. Feature hii mpya ambayo tunaifanyia majaribio kwa sasa itafanya urahisi wa kusupport kwa njia ya malipo na jinsi ya kupakua apps kwa uharaka zaidi kwenye Google PlayStore."
No comments