Kila kitu unachopaswa kujua kuhusu Android 11
Android ni mfumo wa wa ueshaji wa wa s ambao ni maarufu sana duniani kote kwani kampuni nyingi za kutengeneza simu zimekuwa zikitumia mfumo huu, zikiwemo Samsung, Sony, HTC, Tecno na nyingine nyingi. Mfumo huu wa uendeshaji maarufu kama Android umekuwa ukiendelea kuboreshwa siku hata siku ili kumpa mtumiaji urahisi lakini pia kuona ubora na kujivunia kuendelea kutumia mfumo huo.
Android 11 ilitengenezwa kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Februari, na ikawa imerejewa upya mwezi uliopita (Machi) na sasa imerejewa kwa mara ya tatu katika kuuboresha mfumo huo (Developer Preview 3), kabla hawajaamua kuutangaza na kuanza kutumika. Haya ni mambo ambayo tunatakiwa tuyatarajie katika Android 11 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka huu.
Screen Recorder
Google kwa kipindi kirefu sana wamekuwa wakiwaahidi wateja wake kwamba wataleta feature hiyo kwenye simu za Android, lakini sasa kupitia Android 11, inategemea feature hiyo kuwepo na kwa ubora mkubwa. Hapo mwanzo watumiaji wa Android walikuwa wanalazimika kupakua application za kurekodi screen kama vile AZ Screen Recorder na nyingine nyingi kwa sababu hakukuwa na feature hiyo kwenye simu za Android.
Uwezo wa ku'mute notification wakati wa kurekodi video
Mara nyingi sana tumekuwa tukitumia simu zetu kurekodi matukio mbalimbali katika maisha yetu, mengine yakiwa ya kumbukumbu tu na mengine muhimu kabisa kama vile ya kiofisi, sherehe nk, lakini inakuaje pale unapokuwa unarekodu halafu notification ikaingia? Kwa hakika inaboa sana. Kupitia Android 11 sasa utaweza ku'mute notification zote ili kitu unachorekodi kisipate kikwazo chochote.
Ubora wa touch screen
Kama wewe ni moja ya mtu ambae umeweka screen protector kwenye simu yako, kwa hakika utakuwa umewahi kukutana na hili, kuna muda unashindwa au screen inachelewa kupokea touch uliyofanya kwa muda huohuo. Tatizo hili likasababishwa na simu husika lakini mara nyingi huwa ni screen protector. Kupitia Android 11, Google wamehakikisha kuongeza uwezo wa kuhisi wa screen (screen sensitivity) ili kwamba mtumiaji asiwe anapata tatizo lolote wakati anatumia simu yake.
Notification History
Kupitia Android 11 sasa utaweza kuwa na notification history, sehemu ambayo unaweza ukaenda na kuona notification zako zote ulizozipokea kwa siku hiyo, hii itasaidia sana kama labda kuna baadhi ya notification ambazo ulizitoa kwa bahati mbaya na bila kujua kama ilikuwa ya muhimu au kama kuna notification ulisahau kuisoma
Hapo mwanzo, kuwasha airplane mode kulikuwa kunazima Bluetooth jambo ambalo kimsingi halileti maana. Kwa mtu ambaye alikuwa anatumia (bluetooth headphones) alikuwa analazimika kuwasha tena bluetooth ili aendelee kusikiliza muziki au kuendelea na mambo mengine aliyokuwa akiyafanya. Kupitia Android 11, Google wameamua kurekebisha tatizo hilo na sasa ukiwasha Airplane Mode bado Bluetooth itaendelea kuwaka pia.
No comments