Header Ads

Breaking News

Whatsapp inatarajia kuja na feature mpya kwa ajili ya Video Calls

Mtandao wa Whatsapp umeandaa Update ambayo iko mbiona kuja ambao utahusisha features mbalimbali mpya ambazo hazikuwepo hapo mwanzo. Haya ndio mambo unayopaswa kuyafahamu kuhusuana na update hiyo:

Whatsapp wanatarajia kuongeza ubora ubora wa video call zao tofauti na awali. Whatsapp ndio mtandao wa kuchat maarufu zaidi duniani na ambao umepakuliwa na watu wengi sana zaidi ya bilioni 2 duniani kote huku mitandao mingine yenye sifa kama ya mtandao huo ikiwa Skype, FaceTime, Zoom na HouseParty hususani kwenye suala la video call. 

Wakati duniani kote watu wakiwa wamejitenga kutokana na janga la Corona, mitandao ya jamii na video calls zimekuwa msaada mkubwa sana wa kujuliana hali, watu wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kuwajulia hali wapendwa wao pamoja na kuongea mambo muhimu ya biashara hasa mikutano. 

Whatsapp nayo haikuwa nyuma katika hilo, kupitia sehemu yake ya video chat ambayo hapo mwanzo ilikuwa ikilimit namba ya watu wanaoweza kuwasiliana kwa kupitia video call, sasa imeongeza idadi ya watu kufikia hadi watu nane tofauti na hapo awali ambapo mwisho ilikuwa ni watu wanne. 

No comments