Samsung kutumia teknolojia ya AI kuboresha mfumo wa sauti wa TV zake
Samsung ni moja ya kampuni bora na maarufu zaidi duniani kote kwa kutengeneza bidhaa za kielektroniki kama vile simu, redio, na bidhaa nyingine zikiwemo Smart TV maarufu kama QLED ambazo kwa sasa wameziboresha zaidi. Ili kuendana na uboreshaji wa TV hizo, Samsung wanatarajia kuboresha ubora wa sauti katika Tv hizo kupitia teknolojia ya AI (Artificial Intelligence).
Ili kutengeneza mazingira mazuri na ya mandhari kuwa kama uko kwenye sehemu za sinema (cinemax), ndani ya chumba chako, Tv hizo ambazo zinakuja na teknolojia hiyo ya AI zitakuwa na speaker sita za ndani (built in) kwa mfano kama gari ikiwa inatembea kutoka upande wa kushoto wa TV kuelekea upande wa kulia basi speaker hizo nazo zitakuwa zikihamisha sauti kutoka upande wa kushoto wa speaker kuelekea upande wa kulia.
Lakini pia TV hizo zinakuja na teknolojia ya AVA (Active Voice Amplifier) ambayo teknolojia hiyo itakuwa inatumika kwa speaker za nje (external speakers) ili mtumiaji asiwe anapata tabu ya kuongeza sauti au kupunguza mara kwa mara.
Sambamba na hilo Tv hizo zinakuja na sound sensors ambazo zitasaidia kuhisi sauti iliyoko nje. Sensor hizo zitakuwa zikilinganisha sauti kutoka nje na ndani ili kuleta mlingano wa sauti, ikiwa na maana kwamba kama kutakuwa na redio ikilia jikoni au kutakuwa na sauti za radi basi Tv hizo zitaweza kusense sauti za nje na kuongeza sauti zenyewe bila mtumiaji kufanya chochote. Hiyo yote ni katika kuboresha huduma za kampuni hiyo kwa wateja wake.
No comments