Header Ads

Breaking News

Feature mpya YouTube: Sehemu ya chapters kwa ajili ya video ndefu

Ni ukweli usiopingika kwamba moja kati ya vitu vinavyoboa katika YouTube ni kuangalia video ndefu huku ukiwa unapeleka mbele mara kwa mara ili kuweza kuona kile ambacho ndio haswa kimekufanya uangalie video hiyo. Watu wengi wamekuwa wameulalamikia mtandao huo kwani wakati mwingine inawalazimu kuangalia video ndefu sana kuja kugundua kuwa jambo ambalo walikuwa wanataka kuangalia lipo katikati au mwishoni kabisa mwa video hiyo.

Baada ya malalamiko hayo kuzidi kwa muda mrefu, YouTube imeweza kusikia kilio cha watumiaji wake na kwa sasa unaweza kuangalia video yoyote ile kwa sura (chapters) kulingana na dakika ama sekunde za video hiyo. Hivi sasa kadri utakavyokuwa unapeleka mbele video, sura (chapter) itakuwa inatokea kwa chini ya video ili kuweza kukuongesha sehemu hiyo inazungumzia kitu gani hivyo ni rahisi kupeleka mbele kama haikuhusu ama kuangalia kama ndilo hitaji lako. Unaweza ukaangalia mfano wa sehemu hiyo hapa chini;
 Ili kuweza kufanya hivyo kwa wale watengenezaji wa video za YouTube, wanatakiwa waandike maelezo kwenye sehemu ya description wakati wa ku-upload, na sehemu hii itaweza kufanya kazi kwenye video yoyote ile inayoanzia sekunde 10 na kuendelea.

YouTube imeanza kufanya majaribio juu ya sehemu hiyo mpya kwa muda mrefu sasa, hivyo baadhi ya watu huenda watakuwa wameshaiona sehemu hiyo lakini kwa baadhi ya watu ambao bado hawajaiona, wanaweza wakafanya update kwenye application zao. 

No comments