Header Ads

Breaking News

Money Heist Season 5: Lini inatoka, nini cha kutegemea

Series ya kimataifa kutoka Netflix inayofahamika kama Money Heist (La Casa De Papel) ilirejea tena machoni pa watu ikiwa na season ya 4 mwanzoni mwa mwaka huu mnamo mwezi April na tetesi zilizopo ni kwamba series hiyo iko mbioni kuja na season ya 5. 
Hiki ndicho tunachofahamu mpaka kufikia hivi sasa kuhusu season ya 5, lini itatoka na nini tutegemee baada ya season ya 4 kumalizika.

Hivi karibuni tutaskia pia kuhusu takwimu kuhusu namna series hiyo ilivyofanya vizuri maana Netflix huwa wanatoa takwimu hizohizo mara kwa mara, wanapokuwa wanatoa hesabu ya mapato yao kwenye mikutano. Lakini mpaka kufikia sasa, series hiyo ndiyo ambayo inashikilia rekodi kwa kuwa series ambayo imeingiza pesa nyingi pamoja na kutazamwa na watu wengi sana duniani kote ikiwa ni series ambayo lugha yake sio ya kiingereza.

Season 4 ya Money Heist ilitangazwa kwenye Netflix na duniani kote mnamo tarehe 3 April mwaka 2020 na ilikuwa na episodes 8.

Je kutakuwa na season 5?

Kama wewe ni mpenzi wa series hii, nadhani utakuwa umejiuliza hili swali baada ya season ya 4 kuisha, lakini kila dalili inaonesha kuwa kutakuwa na season ya 5 hata vyanzo mbalimbali vya habari nchini Hispania vimeongelea kuhusu tetesi hizo lakini huenda ikawa ni mapema sana kuongelea suala hilo. Lakini sababu ya kufanya tuamini kuwa kutakuwa na season ya 5 ni kama zifuatazo. 
Kwa kuanzia, story bado haijaisha. Japokuwa tutaliongelea hili baadae lakini tukio la wizi wa pili bado halijaisha, hii inamaanisha kuwa tutegemee bado kuna season nyingine moja ili kumalizia story nzima na kutoa maswali ambayo bado yapo mengi kwa watazamaji.

Lakini pia Alex Pina ambae ndiye mtunzi wa story hiyo, amekuwa akisikika mara kwa mara na waandishi wenzake pamoja na ma-director wakiongelea suala la kuwepo season ya 5 kwenye interview mbalimbali.

Pia moja wa waigizaji wa series hiyo Itziar Ituño ambae anafahamika kama Raquel Murillo (Lisbon) kwenye series hiyo alisikika akisema kwenye interview kuwa "nina furaha kwani kwa sasa tunaendelea na kushoot season ya 4 lakini habari mbaya ni kwamba haiishii hapo" hii ni kusema kuwa kwa tafsiri nyingine tutegemee season ya 5. 
Season ya 4 ya Money Heist ilivunja rekodi kwa kutazamwa na watu milioni 65 na bado series hiyo imeendelea kushika vichwa vya habari katika nchi nyingi ikiwemo UK ambako tangu kuzinduliwa kwa season 4 mpaka sasa bado iko miongoni mwa season 5 zinazozidi kuongelewa katika nchi hiyo jambo ambalo si la kawaida.

Kwa kumalizia tu swali kuhusu season ya 5, swali sahihi la kuuliza ni kuwa season ya 5 itatoka lini na sio kama itatoka au la, kwani tumeshafahamu kuwa itatoka hivi karibuni, moja ya changamoto ya kusogeza mbele kushoot kwa season hiyo ni pamoja na janga la corona kama tunavyofahamu, na hispania ikiwa ni moja ya nchi iliyokumbwa na janga hilo kwa ukubwa wake. 

Nini tutegemee kwenye season 5?

Labda tujikumbushe kwa haraka haraka matukio muhimu kwenye season ya 4 na jinsi ilivyofikia tamati. Tulimuona Lisbon akiungana na wenzake kwenye Benki ya Hispania baada ya kutoroshwa kutoka mikononi mwa polisi. Changamoto kubwa ambayo wanayo kwa sasa ni kuhusu Professor ambae amekamatwa na ameshikiliwa bunduki.
Wengi wamekuwa wakimzungumzia mwanamke huyu mwenye mimba, ambae kwa sasa anaonekana amebadilika na wengine hata hudiriki kusema na kuamini kuwa mimba yake sio kweli, kuwa ni jambo la uzushi kwani mara nyingi ameonekana kunywa pombe na kahawa jambo ambalo sio zuri kwa mtoto, na wengine husema kuwa huenda akawa ni mke wa Berlin ambae alionekana kwenye season 4 na kwamba hii yote ni plan.

Tukirudi benki, tunaona timu nzima sasa inaendelea na kazi na wako mbioni kabisa kumaliza. Bado wanaendelea na uyayushaji wa dhahabu ili kuwa katika vipande vidogo vidogo ili waweze kusafirisha kwa urahisi.  Swali kubwa ambalo linakuja ni kuwa je wataweza kuondoka salama, na kama watafanikiwa kuondoka, watawezaje kutumia pesa hizo bila kufahamika walipo ilhali tunajua kwa sasa kuwa wengi wao wanafahamika hata kwa sura, je watawezaje kuzuia kukamatwa kama ambavyo ilitokea mara ya mwisho? 

Unaweza kutuandikia hapo chini kwenye comment section nini ambacho unadhani kitatokea na nini unategemea kukiona kwenye season 5

Lini itatoka Season 5?

Series hiyo inategemewa kuchelewa kutoka kwani suala zima la shooting lilisimamishwa kutokana na corona, hivyo shooting itaendelea kuanzia mwezi wa nane hivyo filamu hiyo inatarajia kurejea machoni mwa watu mwaka 2021, tarehe kamili kuhusu lini na mwezi bado haijatangazwa rasmi.

Kama wewe ni moja ya watu ambao bado hawajaangalia season hiyo ya 4, unaweza ukaipakua hapa chini: 

No comments