Nyimbo 6 bora Afrika Mashariki kwa mwezi May 2020
Na hizi ndizo nyimbo sita zilizofanya vizuri sana Afrika Mashariki kwa mwezi huu wa 5 kutoka kwenye mtandao wa OkayAfrica.
Maya Amolo "Jokes"
Mwimbaji wa R&B kutokea nchini Kenya, hivi karibuni aliachia nyimbo yake ya pili kutoka kwenye EP yake iliyotoka mwezi huu wa tano. Mwimbaji huyo anasema aliandika nyimbo hiyo akielezea hali halisi ambayo huwa inatokea kwenye mahusiano, pale ambapo unakuwa na mpenzi wako ukagundua kuwa sio mwaminifu, anatoka na mtu mwingine na unashindwa kufanya lolote juu ya jambo kama hilo na sababu zikiwa ni nyingi ambazo amejaribu kuelezea kwenye nyimbo hiyo.
Ibraa Ft. Harmonize "One Night Stand"
Kutoka KONDEGANG msanii wa kwanza kusainiwa kwenye record label hiyo anayefahamika kama Ibraa, ametoa nyimbo yake ya kwanza akiwa ameshirikisha boss wake Harmonize, nyimbo hiyo ni moja kati ya nyimbo nne za kwenye EP yake anayotegemea kuiachia hivi karibuni. Wasanii wengine wanaosemekana kushirikishwa kwenye EP hiyo ni Joeboy na Skiibii.
Zuchu "Nisamehe"
Msanii mpya kutokea Afrika Mashariki kwenye kundi la WCB Wasafi Zuchu alitoa nyimbo yake ya Nisamehe mwezi huu wa tano. Nyimbo hiyo ni nyimbo ya pili kwenye list ya nyimbo kutoka kwenye EP yake I Am Zuchu ambayo tayari inafanya vizuri sana na imemtambulisha vyema akiwa kama ni msanii wa kuangaliwa sana mwaka huu.
Rayvanny "Sukuma Ndinga"
Hakuna yeyote anayeweza kusema kuwa Rayvanny hana kipaji. Amekuwa akionyesha kipaji chake siku hata siku na jinsi anavyokuwa kwenye mziki. Star huyo kutokea WCB alitoa single nyingine inayoitwa Sukuma Ndinga" ambayo imechanganya miondoko ya Bongo fleva na Trap
Sheebah "Nyakyuka"
Mwimbaji wa Pop kutokea nchini Uganda Sheebah, mwezi huu alitoa nyimbo yake "Nyakyuka" ambayo inaelezea ambayo inaelezea story yake na jinsi alivyokutana na mwanaume aliyebadilisha maisha yake. Kutokana na nchi hiyo kuwa katika lockdown, mwimbaji huyo aliamua kufanya video kwake na akitupa tour ya ndani kwake.
Sauti Sol "Insecure"
Wakati tukisubiri uzinduzi wa albam yao ya tano, bendi hiyo kutokea Kenya Sauti Sol imetuletea nyimbo mpya Insecure
No comments