Header Ads

Breaking News

Vodacom yapunguza tozo kwa baadhi ya tovuti za masomo ili kusaidia wanafunzi kujisomea


Kutokea jijini Dar es Salaam, Mtandao wa simu nchini Tanzania unaofahamika kama Vodacom, umeweka jitihada za kupunguza gharama za tozo katika baadhi ya tovuti za masomo na tovuti nyingine kutotozwa gharama yoyote ile pale mwanafunzi anapokuwa anatembelea tovuti hizo ili kuwawezesha wanafunzi kupata urahisi wa usomaji hususani katika kipindi hiki kigumu cha janga la corona.

Mtandao huo wa simu umeshirikiana na baadhi ya shule pamoja na vyuo hapa nchini kuhakikisha kwamba wanafanikisha jambo hilo la muhimu. Baadhi ya taasisi hizo ni: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi ya Afya ya Mkolani, Chuo Kikuu cha St. Joseph nchini Tanzania, ikiwemo na vyuo mbalimbali vya afya pamoja na shule.



Kampuni hiyo imesema katika taarifa jana kuwa inaona watu wengi wameanza kusoma kwa njia ya mtandao, mikusanyiko inapungua, burudani za nyumbani, na hali ya kufanya kazi kupungua jambo ambalo linatokea duniani kote. Hii inaonesha namna ambavyo mtandao unahitajika na umuhimu wake ili biashara ziweze kuendelea kama kawaida, shughuli za shule na jamii iendelee kuwasiliana na wapendwa wao.
Jitihada hizi zilizofanywa na kampuni ya Voda zitaenda kunufaisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu, waalimu, wahadhiri n wazazi nchini kote.

"Tumefanya hivi kwa nia njema, tunataka tuwasaidie Watanzania ili waweze kuendelea kuwasiliana pamoja na kujuliana hali lakini huku wakiendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato. Tunaamini kuwa teknolojia ni jukwaa linaloweka na kutoa fursa kwa ajili ya kila mmoja kufikia uwezo wake kamili" alisema Mkurugenzi wa maswala ya mahusiano Vodacom, Ms. Rosalynn Mworia.

Hapo nyuma, Vodacom iliwahi kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Universal Communications Service Access Fund, Dlab pamoja Samsung kwa ajili ya kufanikisha suala hili la elimu kupitia mtandao au elimu kwa njia ya kidigitali kama ambavyo imezoeleka na watu wengi.

Wateja wa Vodacom na kwa wale ambao sio wateja wa mtandao huo, wanaweza pia wakasoma matilio mbalimbali ya shule kupitia Vodacom Instant School - ambalo ni jukwaa kwa ajili ya masomo/kujifunza mtandaoni na linalotoa mafunzo kwa waalimu na wanafunzi kupitia simu janja (smartphone) au computer. Jukwaa hili linapatikana kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari bure kabisa.

No comments