Header Ads

Breaking News

Aga Khan yazindua App kwa ajili ya kupima dalili za corona

Habari njema kwa Watanzania ni kuwa kwa sasa wanaweza wakagundua dalili za gonjwa kubwa la homa ya mapafu au Corona ambalo bado linaendelea kuumiza vichwa duniani kote. Shukrani ziende kwao Hospitali ya Aga Khan wakishirikiana na chuo cha Aga Khan (Aga Khan University).

Taasisi hizo mbili kwa kushirikiana, zimetengeneza application ya kwenye simu janja (smartphone) za aina zote yaani Android na iPhone ambayo inamuwezesha mtumiaji kugundua dalili za ugonjwa huo kwa kufanya scanning ili kusaidia kugundua na namna ya kufanya endapo mtumiaji atakutwa na maambukizi. Application hii inafahamika kwa jina la "Coronachek" na kwa sasa inapatikana katika masoko yote mawili yaani Appstore na Playstore ikiwa ni bure kabisa.
Mkuu wa kituo hicho cha kutoa huduma ya Afya cha Aga Khan, Sisawo Konteh anasema jambo ambalo lilikuwa linasumbua watu wengi ni namna ambavyo ugonjwa huo umekuwa ukiharibu fikra na mtazamo wa watu wengi kupitia taarifa za vifo ambavyo vimekuwa vinaendelea kutangazwa kila leo. Lakini kwa kupitia app hiyo, sasa utaweza kugundua dalili na hivyo utaongozwa namna ya kufanya ili kufikia wataalamu, lakini pia hiyo itasaidia kuondoa mtazamo potofu ambao watu wengi wamekuwa nao kuhusu ugonjwa huo ya kwamba kila anayeupata ni lazima aage dunia.

Application hiyo inatumia teknolojia ya AI yaani Artificial Intelligence na hivyo kwa ndani ya app hiyo kuna chatbot ambae yeye huwa anafanya kazi ya kujibu maswali mbalimbali yanayokuwa yanaulizwa na mtumiaji kwa uharaka kwa hali ya juu. Application hiyo pia inasaidia kuelimisha watanzania wengi kwani ndani ya app hiyo kuna video mbalimbali za wataalamu wa afya wakielezea namna ya kujikinga na maambukizi lakini pia inapunguza msongamano wa watu wengi kwenye vituo vya afya kwajili ya kucheki afya zao

No comments