Cheza game kwenye simu yako kwa kutumia PS4 Controller
Watu wengi hupenda kucheza games kwenye simu zao kwani ni watu wachache wenye uwezo wa kumiliki PlayStation au Xbox kutokana na gharama zao kuwa kubwa. Lakini je, unafahamu kuwa unaweza ukacheza games kwenye simu yako au Tablet yako ya Android kwa kutumia PS4 controller? Ndio, inawezekana kabisa na hatua za kufata ili kuunganisha wala hata sio ngumu. Hatua zenyewe ni kama ifuatavyo:
JINSI YA KUUNGANISHA PS4 NA SIMU AU TABLET YAKO YA ANDROID
Ukiwa unahitaji kuunganisha simu yako na PS4 kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa PS4 controller yako iko katika "Pairing Mode" na ili kufanya hivyo lazima PS4 na PS4 controller zote ziwe zimezimwa.
1. Kama zote zitakuwa tayari zimezimwa, utaanza kubonyeza kitufe (button) ya PS kwenye PS contoller yako, utaibonyeza na kuhold pamoja na kitufe (button) iliyoandikwa "Share" kwa pamoja. Kama utakuwa umefanya kwa usahihi basi utaanza kuona mwanga mbele ya controller yako.
2. Kisha utachukua simu yako ya Android au Tablet, na kuhakikisha kuwa Bluetooth iko ON. Utafungua "Quick Menu" ya simu yako na kwenda palipoandikwa Bluetooth utabonyeza kitufe hicho na kukishikilia (hold).
3. Kama tayari utakuwa umewasha Bluetooth basi kwa chini utaweza kuona "Wireless Controller" tayari kabisa kwa ajili ya kujiunga nayo, au kama itakuwa bado haionekani basi utaweza kuscan na baadae utaiona ikitokeza kwa chini kama inavyoonekana hapo.
4. Baada ya kuwa umefanya hvyo basi utabonyeza OK ili kukamilisha zoezi hili.
Lakini pia inapaswa ufahamu ya kwamba sio kila game la kwenye simu litakubali process hiyo.
No comments