Game ya Fortnite sasa kupatikana kwenye Android
Game hii sio mpya bali ni game maarufu sana kwa wapenzi wa kucheza game. Game hii ilikuwa inapatikana kwenye store ya Epic Games za Samsung Store peke yake na wala haikuwepo PlayStore.
Tatizo pekee lililokuwepo kwa watumiaji wa Android, ni kwamba game hii haikuwa ikipatikana Playstore hivyo mtu aliyekuwa na simu nyingine tofauti na Samsung hakuweza kuwa na game hiyo. Lakini sasa game hiyo unaweza ukaipata kwenye PlayStore na kuidownload kwa free kabisa.
Watengenezaji wa game hiyo, hapo mwanzo hawakuwa wameiweka game hiyo kwenye PlayStore kutokana na kushindwa kuelewana kwenye maswala ya mikataba na Google Play Store, kwani Playstore walikuwa wanahitaji Fortnite wawalipe asilimie 30 ya mapato yote.
Baada ya miezi 18 tangu kuanzishwa kwa game hiyo na kutumika nje ya Playstore, Fortnite sasa wamefanya maridhiano na Google na kuwezekana kuweka game hiyo kwenye Playstore. Google hutumia njia mbalimbali ikiwemo kuzuia application ambazo zinapatikana nje ya Playstore, kutoa onyo na tahadhari kwa mtumiaji endapo atataka kudownload au kuinstall kwa kutoa athari ambazo zinaweza kujitokeza endapo utaendelea na zoezi unalolifanya.
Mpaka kufikia sasa game hiyo tayari imeshadownloadiwa na zaidi ya watu 500,000 licha ya kuwa hata haijafikisha wiki moja tangu kuwekwa kwenye PlayStore
No comments